No Widget Added

Please add some widget in Offcanvs Sidebar

Shopping cart

Subtotal $0.00

View cartCheckout

UPCOMING PROJECT: FAZA BEN

A Psychological Horror / Spiritual Thriller
Produced by:Ravens Studio Tanzania
Duration: 120 Minutes

UFUPISHO
Faza Ben inafuatilia maisha ya kasisi wa Kikatoliki ambaye baada ya tukio la uhalifu kutokea kanisani kwake, anapoteza amani ya moyo na akili. Anaanza kupambana na maono, sauti, na mashaka ya kiroho yanayomfanya ashindwe kutofautisha kati ya uhalisia na ndoto za kichaa. Kadri anavyozama kwenye dunia yake ya kiakili, anaanza kuwaona waumini kama pepo waliovaa ngozi ya binadamu jambo linaloelekea kuvunja mpaka kati ya imani, wazimu, na wokovu.

Mwisho wa safari yake unaacha maswali mazito:

  • Imani bila afya ya akili inaweza kuwa sumu.
  • Je, mtu anawezaje kumpa Mungu moyo uliojaa majeraha ambayo hajayasamehe?

Key Messages

  • Watumishi wa Mungu pia ni binadamu wanaoweza kuumia.
  • Msamaha wa kweli huanza kwa kujisamehe mwenyewe.
  • Imani na akili lazima ziishi kwa usawa.
Blog Image

BEHIND THE SCENES / CASTING CALL – COMING SOON

Ravens Studio inatayarisha kipindi maalum cha nyuma ya pazia (Behind the Scenes) cha filamu ya Faza Ben, kitakachoonyesha safari ya uzalishaji, mahojiano na waigizaji, na changamoto halisi za kurekodi filamu ya kiroho yenye maudhui mazito.

Taarifa za rasmi za Casting Call (majaribio ya waigizaji) yatatangazwa hivi karibuni. Ikiwa una kipaji cha uigizaji, sauti, au unataka kujifunza kuhusu ulimwengu wa filamu jiandae kushiriki

SPONSORSHIP & BRAND PLACEMENT OPPORTUNITIES
Faza Ben ni zaidi ya filamu ni jukwaa la kipekee kwa makampuni, bidhaa na taasisi kujionyesha mbele ya maelfu ya watazamaji.

Kwa wafadhili au wadau watakaounganisha nguvu nasi:

  • Logo au bidhaa yako inaweza kuonekana ndani ya filamu (Brand Placement).
  •  Utatajwa kwenye credits, trailers, na mawasiliano yote rasmi ya promosheni.
  • Utapata ofa maalum ya kufanyiwa usimamizi wa website yako bure kwa mwaka mmoja (kwa udhamini kuanzia milioni 2 TZS na kuendelea).
  •  Pia, utajumuishwa kwenye vipindi vya matangazo kabla na baada ya filamu.


SHIRIKI NASI LEO!
Wachezaji wa filamu (Actors & Actresses)
Wadau wa matangazo (Brands & Sponsors)
Wataalamu wa production (Cinematographers, Makeup Artists, Sound Designers n.k.)

Wasiliana nasi kwa maombi ya ushiriki au udhamini:
📧 [email protected]
🌐 www.ravens.co.tz
📞 ‪+255 692111102‬

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Gravatar profile